Monday, September 2, 2019

SICHEZEWI KIMWILI WALA KIAKILI

Aug 31, 2019 Taasisi yako ya All for Zanzibar Children Association ilifanikiwa kutoa elimu ya “jinsi ya kujiweka mbali na udhalilishaji wa kijinsia” kwa watoto, katika skuli ya Jabal Hiraa iliyopo Fuoni kisiwani Unguja.

Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa “SICHEZEWI KIMWILI WALA KIAKILI” unaotekelezwa na taasisi hii ambao una dhamira ya kutembelea skuli na madrasa zote za Unguja na Pemba na zoezi hili limeshaanza kutekelezwa ipasavyo, lengo ni kuwapa taaluma watoto kukaa mbali na viashiria vya udhalilishaji, lakini hata walimu kuwa makini kwa wanafunzi wao.