Monday, September 9, 2019

Mradi wa SICHEZEWI KIMWILI WALA KIAKILI watua kwa walemavu wa uziwi.


Katika mwendeleo wa utoaji elimu kwa watoto Juu ya jinsi ya kujiweka mbali na udhalilishaji mara hii taasisi ya AZCA ili bahatika kutoka taaluma hiyo katika kituo cha kusomesha lugha ya alama kwa watoto viziwi huko Mwanakwerekwe kisiwani Unguja,Alhamdulillah watoto wamefurahika sana juu ya elimu hii, kumbuka hii ni huu ni mradi wa "sikubali kuchezewa kiakili wala kimwili"

Mshauri mkuu wa AZCA Hidaya Mohd akitoa mafunzo ya athari za kudhalilishaji, huku akiwataka watoto hao kuripoti kila wanachokiona kibaya kwao,waripoti kwa wazazi wao au kwa walimu wao.


Picha ya pamoja baina ya wanafunzi,walimu na uwongozi wa taasisi ya AZCA mara baada ya mafunzo hayo kumalizia,watoto walifurahia mafunzo hayo na wote walionekana kuwa tayari kuripoti matendo hayo machafu.

No comments:

Post a Comment