Mwezi mmoja nyuma (Mwezi wa tano ) mwaka huu , tasisi ilipokea taarifa za ugonjwa wa mtoto mdogo(Khalfan Suleiman ) kutoka Wambaa mkoa wa kusini Pemba, tokea alipozaliwa hawezi kwenda haja kubwa mpaka kutumike dawa maalum ndipo afanikishe shuhuli hiyo.
Hivyo mama mzazi analazimika kumkisia mwanawe kuwa sasa anata kwenda haja ndipo atumie dawa hiyo.
Taasisi ya AZCA ilimfuatilia mtoto huyu kwa wahisani mbambali na hatimae amekuja kisiwani Unguja kwa matibabu Zaidi na hadi sasa tunaendelea nae mpaka pale tutakapoona hali yake imeimarika na kuwa nzuri.
Hali ya maisha kiuchumi kwa mama wa mtoto huyu ni mbaya hivyo tumeamua kulivalia njuga suala hili kwa lengo la kuisaidia familia hiyo, kadhalika pia tunakuomba kutoa mchango wako ili mtoto huyu azidi kufanikisha matibabu yake kwani mahitaji ni mengi sana yanayotakiwa na taasisi haina pesa Zaidi ya kwa wadau kama wewe unaesoma ujumbe huu, njoo tuungane pamoja kumshuhulikia mtoto huyu, fahari yetu kumuona mtoto anakuwa imara kiafya, leo kwake kesho kwako ona kama limekufika wewe.
Unaweza kutuma mchango wako kwa nambari ya simu 0772 99 70 18 / 0717 66 77 70 kisha tuambie umemkusudia nani, au tumia nambari hizo hizo kwa mawasiliano Zaidi.
Aliyembebda mtoto ni Ali Mjomba Dawa Mwanachama wa All for Zanzibar Children Association – AZCA , tulipokwenda kumtembelea na kumfariji huko ZIWATUWE AMANI alipofikia kutoka Pemba
No comments:
Post a Comment