Jumuiya ya kuwasaida watoto Zanzibar (All for Zanzibar Children Association AZCA) ni taasisi iliyosajiliwa rasmi na serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Reg No Z00000014934 on 24/13/2018 Through Act No 6 of 1995) kwa lengo la kuwasaidia watoto waliyo katika mazingira magumu na hata wanaoishi katika mazingira ya kawaida kuwaelekeza mwendendo bora wa kuyafikia malengo sahihi katika maisha.
Miongoni mwa kazi za taasisi, ni kuibua changamoto zinazowakabili watoto kwa lengo la kuionyesha jamii ili kutoa msaada katika kuondosha changamoto hizo, kutoa misaada ya moja kwa moja, kusaidia katika kukuza ufaulu wa watoto skuli, madrasa na kwengineko.
Tunawakaribisha wote watakaotaka kufanya kazi na nasi na itakapotokea popote kuna mtoto anakosa haki zake za msingi kama vile elimu, afya nk usiache kuwasiliana nasi kwa nambari za simu tulizokuwekea.
Mawasiliano : +255717667770 / +255774181532/+255624432662/+255777374545
No comments:
Post a Comment