
Naibu Katibu mkuu wa All for Zanzibar Children Association - AZCA Salama Said Aboud akiwa makini kusikiliza kinacho changiwa na wanakamati tendaji wa jumuiya katika kikao kilicho fanyika jana tarehe 07 july 2019 huko Vuga Mjini Zanzibar.
Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ikiwamo suala la kutafuta "jumuiya washirika" wenye malengo yanayofanana na taasisi ya AZCA.
Mwisho katika mkutano huo uliyowashirikisha wajumbe wa kamati tendaji hao , Naibu katibu Mkuu Salama Said aliwataka watendaji wote wa jumuiya
kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia mafunzo na taaluma wanayopeana kila siku , kwani hali hiyo itawafanya wawe wenye kupiga hatua mbele za kimaendeleo na isiwe kama watu waliyo lala usingizi.
Picha hii imepigwa na Salmin Juma Salmin -Afisa habari wa jumuiya ya AZCA.
Wakwanza ni Suleiman Khamis Haji Katibu mkuu wa Jumuiya ya All for Zanzibar Childrean na wa pili ni Hidaya Ali Muhamed ambae ni Mshauri mkuu maadili wa taasisi hii.
Ni katika mkutano uliyowakutanisha wajumbe wote wa kamati tendaji wa jumuiya , kama malengo yalivyokwisha elezewa huko juu kwa Naibu Katibu mkuu , mkutano huo pia ulitoka na azma nyengine ya kuongeza wanachama ambapo, hatua za kukidhi matakwa ya kisheria zitakapokamilika , taarifa zitatolewa kwa umma kuruhusu watu wa makundi tofauti kujiunga na taasisi kwa lengo na shabaha ya kuiinua jumuiya na hatimae kila mtoto aliyekusudiwa kupatiwa haki zake zote zinazompasa kuzipata kisheria
Picha hii imepigwa na Salmin Juma Salmin -Afisa habari wa jumuiya ya AZCA.
No comments:
Post a Comment