Assalam Alykum Warahmatullahi Wabarakatuh?
Hawa ni watoto kutoka kijiji cha Junguni, Wete Kisiwani Pemba
nchni Tanzania (Zanzibar) ambao ni Husna na Riziki Hamadi , mmoja wa miaka 19
na mwengine miaka 6.
Siku chache zilozopita walipatwa na homa, badae wakaanza kuoza
macho kisha uso na mwili wote, wazazi
wameshafuatilia matibabu katika hospitali tofauti lakini imeshindikana hasa
kwakua hawana pesa za kujikimu katika matibatu.
Hali za familia ya watoto hawa kiuchumi ni mbaya sana, tunakuomba
msaada wako kuchangia fedha kwa lengo la kuwapatia matibabu hata ikiwezekana
nje ya nchi, tatizo kubwa ni hali mbaya kifedha na kama una uwezo wa kuwafanyia
mpango matibabu wewe pia unakaribishwa.
Taasisi yako ya AZCA inabeba jukumu la kukuomba msaada kwa watoto hawa baadae kuwashuhulikia matibabu ili waendelee kuishi kwa Amani, kwani bado wanahitaji kusoma na kuishi vizuri, changia kwaajili ya ALLAH SUBHAANAHU WATAALA, SADAKA YAKO UTAIKUTA MBELE YA MUNGU.
Mawasiliano +255774181532 / +255774253759
Nambari ya kuchangia pesa (tigo pesa) +255672560173
No comments:
Post a Comment