Thursday, August 15, 2019

TAARIFA KWA WASOMAJI, WAFUATILIAJI NA KILA ANAETAKA KUJUA KUHUSU WATOTO WAGONJWA TULIYO WATOA PEMBA KWAAJILI YA KUWAPATIA MATIBABU.


Assalam Alykum Warahmatullahi Wabarakatuh ?

Awali ya yote tuna mshukuru Muumba kutupa nguvu ya kulisimamia hili.

Watoto wetu tuliwafikisha katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja Unguja kwa matibabu na Alhamdulillahi walifanyiwa huduma kadiri ilivyowezekana hapo.

Siku mbili nyuma, yaani juzi baada ya hatua kukamilika tulifanikiwa kuwasafirisha wote watatu pamoja na wazee wao hadi katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo hadi hivi sasa wanaendelea kupokea matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.


Tunakujuza taarifa hii ili tu ujue kinachoendelea na taarifa rasmi itafutia baada ya hatua zote kukamilika.

Watoto hao wapo chini ya usimamizi wa taasisi ya ALL FOR ZANZIBAR CHILDREN ASSOCIATION – AZCA na inahakikisha wanapata huduma nzuri za matibabu.

Taasisi inawashukuru wale wate waliyojitokeza kutoa michango yao ya hali na mali kufanikisha kupatiwa matibabu haya, ahsanteni na hongereni sana, lakini pia musituache mkono kwani safari hii ya matibabu ni ndefu sana.

Baadae tutatoa tena taarifa nini kinatakikana.
Ahsanteni

Imetolewa na
Afisa habari na uhusiano
All for Zanzibar children association – AZCA

No comments:

Post a Comment