Mara
nyingi unaposikiliza vyombo vya habari hukosi kusikia tukio la udhalilishaji
dhidi ya wanawake na watoto nchini Zanzibar, tatizo hili linaonekana kuwa kubwa
kiasi, hivyo taasisi ya AZCA imeamua
kubuni kila njia kuhakikisha inasaidia kuondosha tatizo hili ambalo wahanga
wakubwa ni watoto na mamazao.
Ingawa
juhudi hizo zimenza katika nyanja tofauti kama vile kupita madrasa kutoa
taaluma ya kujiweka mbali na udhalilishaji nk. pia taasisi imepata nafasi ya
kushirikia katika kituo cha radio swahiba fm na kutoa taaluma hiyo kwa jamii.
Ni
imani yetu wanajamii walitusikia vyema na matumaini yetu kila mmoja awe mwalimu
kwa mwenzake kumuhamasisha kupiga vita matukio haya mabaya ya udhalilishaji
yanawakosesha haki za msingi watoto kama
vile haki ya elimu na kutembea.
No comments:
Post a Comment