Sunday, July 28, 2019

“ SITAKI KUCHEZEWA KIMWILI WALA KIAKILI”

Kumekua na titizo kubwa ambalo linaendelea kuisokota nchi, familia na hata mtu mmoja mmoja , ni tatizo la udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Mara nyingi kuna sikika watoto kubakwa, kupigwa vipigo vizito, matusi na aina nyengine za kashfa.
Kutokana na kushahididi matukio haya , wadau mbalimbali wamekua wakijitokeza kusaidia kuondosha matatizo haya, nasi ni miongoni mwao tumeamua kujikita zaidi kielimu, tumeanza na mpango kazi wetu wa kutembelea madrasa mbalimbali visiwani Unguja kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na udhalilishaji kwa wanafunzi na walimu.

Jana tarehe 27 July 2019 tulifanikiwa kutoa elimu katika Al-madrasatul Muhaajirina iliyopo huko Mwera wilayani - Zanzibar.

Tunamshukuru Mungu tumepokewa vizuri na hadi tunaondoka tumejiridhisha kuwa wanafunzi na walimu wao wametufahamu tulichokusudia kuwaambia ambacho ni “kuishi bila ya udhalilishaji inawezekana” na tumeacha msemo ili kujikumbushia elimu tuliyowapa , msemo usemao “ SITAKI KUCHEZEWA KIMWILI WALA KIAKILI”

Katika mchakato huu wa kupita madrasa hadi madrasa pia tunatarajia kutembelea katika madrasa za huko Kiswani Pemba muda mchache baadae.

Unakaribishwa kuungana nasi , tumia mawasiliano yetu yanayopatikana kupitia ukuta huuu.

No comments:

Post a Comment