Monday, August 12, 2019

SAIDIA YATIMA HUPOTEZI BALI UNAWEKEZA SIKU YA MALIPO


Inafahamika kuwa  kipindi cha Skukuu   kila mmoja anatakiwa awe na furaha ili mambo yaende sawa, chakusikitisha kuna makundi ya watu katika jamii tunazoishi wanafikiwa na skukuu wakiwa hawana furaha kabisa, likiwamo kundi la Watoto yatima.


Kiuhalisia, uyatima unauma, lakini unazidi kuuma sana  katika masiku kama haya, mtoto anawaza siku  ya leo angaekuwepo baba angekua ameshapata nguo, "angekuwepo baba ningepata pesa" hasa akiwaona wenzake wamependeza na kwenda viwanjani.

Shukran za dhati zimfikie aliyejitokeza kuchangia kutoa vitambaa vya kushonewa nguo watoto wayima ili wajihisi kuwa si watofauti na wawe na furaha, tunamshukuru mungu jukumu hili tumelisimamia vizuri na siku  mbili kabla ya skukuu tuliwapatia vitambaa hivyo watoto yatima ambao tunawasimamia, tunakuomba nawe mwenye nguo hata za mtumba, toys za kuchezea, pesa, nk tuletee, jicho lao ni sisi , changia ili kuwafanya wawe na furaha, hawana pakuendea isipokua kwa waisilamu wenzao, njoo ujenge pepo yako kwa kuwaokoa watoto yatima.

Nambari zetu kama zinavyoonekana mtandaoni na hapa tunakuwekea..+255774181532/+255624432662/+255777374545

ACNT : NMB NO:  22910033046 Jina: All For Zanzibar Children Association



Mwanamke ni Hidaya Mohammed na Mwanaume ni Ali Mjamba maafisa wa AZCA wakivipima vitambaa vilivyotolewa kwaajili ya kuwapa watoto yatima na baadae kuvikata ili kuwapa watoto hao kwa mujibu wa vipimo vilivyotakiwa.


No comments:

Post a Comment