ALL FOR ZANZIBAR CHILDREN ASSOCIATION (AZCA)
"tunajali kwa kila hali"
Monday, September 9, 2019
Monday, September 2, 2019
SICHEZEWI KIMWILI WALA KIAKILI
Aug 31, 2019 Taasisi yako ya All for Zanzibar Children Association ilifanikiwa kutoa elimu ya “jinsi ya kujiweka mbali na udhalilishaji wa kijinsia” kwa watoto, katika skuli ya Jabal Hiraa iliyopo Fuoni kisiwani Unguja.
Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa “SICHEZEWI KIMWILI WALA KIAKILI” unaotekelezwa na taasisi hii ambao una dhamira ya kutembelea skuli na madrasa zote za Unguja na Pemba na zoezi hili limeshaanza kutekelezwa ipasavyo, lengo ni kuwapa taaluma watoto kukaa mbali na viashiria vya udhalilishaji, lakini hata walimu kuwa makini kwa wanafunzi wao.
Thursday, August 15, 2019
TAARIFA KWA WASOMAJI, WAFUATILIAJI NA KILA ANAETAKA KUJUA KUHUSU WATOTO WAGONJWA TULIYO WATOA PEMBA KWAAJILI YA KUWAPATIA MATIBABU.
Assalam
Alykum Warahmatullahi Wabarakatuh ?
Awali ya yote tuna mshukuru Muumba kutupa nguvu ya
kulisimamia hili.
Watoto wetu tuliwafikisha katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja
Unguja kwa matibabu na Alhamdulillahi walifanyiwa huduma kadiri ilivyowezekana
hapo.
Siku mbili nyuma, yaani juzi baada ya hatua kukamilika
tulifanikiwa kuwasafirisha wote watatu pamoja na wazee wao hadi katika
hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo hadi hivi sasa wanaendelea
kupokea matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Tunakujuza taarifa hii ili tu ujue kinachoendelea na taarifa
rasmi itafutia baada ya hatua zote kukamilika.
Watoto hao wapo chini ya usimamizi wa taasisi ya ALL FOR
ZANZIBAR CHILDREN ASSOCIATION – AZCA na inahakikisha wanapata huduma nzuri za
matibabu.
Taasisi inawashukuru wale wate waliyojitokeza kutoa michango
yao ya hali na mali kufanikisha kupatiwa matibabu haya, ahsanteni na hongereni
sana, lakini pia musituache mkono kwani safari hii ya matibabu ni ndefu sana.
Baadae tutatoa tena taarifa nini kinatakikana.
Ahsanteni
Imetolewa na
Afisa habari na
uhusiano
All for Zanzibar
children association – AZCA
Monday, August 12, 2019
PINGA UDHALILISHAJI , NI ADUI WA HAKI ZA WATOTO.
Mara
nyingi unaposikiliza vyombo vya habari hukosi kusikia tukio la udhalilishaji
dhidi ya wanawake na watoto nchini Zanzibar, tatizo hili linaonekana kuwa kubwa
kiasi, hivyo taasisi ya AZCA imeamua
kubuni kila njia kuhakikisha inasaidia kuondosha tatizo hili ambalo wahanga
wakubwa ni watoto na mamazao.
SAIDIA YATIMA HUPOTEZI BALI UNAWEKEZA SIKU YA MALIPO
Inafahamika
kuwa kipindi cha Skukuu kila mmoja anatakiwa awe na furaha ili mambo
yaende sawa, chakusikitisha kuna makundi ya watu katika jamii tunazoishi
wanafikiwa na skukuu wakiwa hawana furaha kabisa, likiwamo kundi la Watoto
yatima.
Kiuhalisia,
uyatima unauma, lakini unazidi kuuma sana
katika masiku kama haya, mtoto anawaza siku ya leo angaekuwepo baba angekua ameshapata
nguo, "angekuwepo baba ningepata pesa" hasa akiwaona wenzake
wamependeza na kwenda viwanjani.
Subscribe to:
Posts (Atom)