Wednesday, June 26, 2019

Matukio katika safari kumfariji mama wa mtoto mgonjwa


Mshauri Mkuu wa AZCA apeleka zawadi kwa mgonjwa.

Kushoto ni Mshauri mkuu wa Jumuiya ya kusaidia watoto Zanzibar (AZCA) Hidaya Ali Muhamed akimkabidhi Bi Fadhila Malik Juma zawadi ya Pempas zilizotolewa na taasisi hii.

Tukio hili ni la jana 25 june 2019 huko ZIWATUWE  Amani Zanzibar baada ya jumuiya kumsafirisha mama huyu ambae mwanawe anasumbuliwa na kutopata choo tokea kuzaliwa kuja kisiwani Unguja kwaajili ya Matibabu.

Mtoto huyo anaesumbuliwa na ugonjwa huo anaumri wa mwaka mmoja na miezi 5 na alianza tukio hilo tokea siku alipozaliwa na taasisi yako Pendwa jana ilimtembelea kwa lengo la kumfariji pamoja na kufanya nae mazungumzo juu ya kinachotakiwa katika matibabu ya mtoto.

Mwekekiti wa tasisi ya kusaidia watoto Zanzibar akionyesha dawa

Mwenyekiti wa AZCA, Bahiya Bakari Aly akionyesha dawa maalum anayotumia mtoto mwenye tatizo la kutopata choo na hadi atumie dawa hiyo ndipo haja kubwa itoke.

Ilikua jana ambapo taasisi hii ilikwenda kumetembelea mtoto huyo huko ZIWATUWE AMANI kisiwani unguja.

Kuhusu Jumuiya

Jumuiya ya kuwasaida watoto Zanzibar (All for Zanzibar Children Association AZCA) ni taasisi iliyosajiliwa rasmi na serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Reg No Z00000014934 on 24/13/2018 Through Act No 6 of 1995) kwa lengo la kuwasaidia watoto waliyo katika mazingira magumu na hata wanaoishi katika mazingira ya kawaida kuwaelekeza mwendendo bora wa kuyafikia malengo sahihi katika maisha.

Miongoni mwa kazi za taasisi, ni kuibua changamoto zinazowakabili watoto kwa lengo la kuionyesha jamii ili kutoa msaada katika kuondosha changamoto hizo, kutoa misaada ya moja kwa moja, kusaidia katika kukuza ufaulu wa watoto skuli, madrasa na kwengineko.

Taasisi inapatikana Kisauni mkoa wa Mjini Maghribi Unguja.

Taasisi imefika kumfariji mtoto mwenye tatizo la kutopata choo

Mwezi mmoja nyuma (Mwezi wa tano ) mwaka huu , tasisi ilipokea taarifa za ugonjwa wa mtoto mdogo(Khalfan Suleiman ) kutoka Wambaa mkoa wa kusini Pemba, tokea alipozaliwa hawezi kwenda haja kubwa mpaka kutumike dawa maalum ndipo afanikishe shuhuli hiyo.

Hivyo mama mzazi analazimika kumkisia mwanawe kuwa sasa anata kwenda haja ndipo atumie dawa hiyo.

Taasisi ya AZCA ilimfuatilia mtoto huyu kwa wahisani mbambali na hatimae amekuja kisiwani Unguja kwa matibabu Zaidi na hadi sasa tunaendelea nae mpaka pale tutakapoona hali yake imeimarika na kuwa nzuri.