Sunday, July 28, 2019

“ SITAKI KUCHEZEWA KIMWILI WALA KIAKILI”


Naibu Katibu Mkuu wa AZCA Bahiya Bakari Ali ambae pia ni Msomi wa fani ya Ustawi wa Jamii akitoa mada ya wanafunzi juu ya maana ya udhalilishaji


Muwasilishaji mada ya VIASHIRIA VYA UDHALILISHAJI kutoka AZCA Ali Mjanga akiwafahamisha wanafunzi namna ya kugundua viashria hivyo na mbinu za kuviepuka.

“ SITAKI KUCHEZEWA KIMWILI WALA KIAKILI”

Kumekua na titizo kubwa ambalo linaendelea kuisokota nchi, familia na hata mtu mmoja mmoja , ni tatizo la udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Mara nyingi kuna sikika watoto kubakwa, kupigwa vipigo vizito, matusi na aina nyengine za kashfa.
Kutokana na kushahididi matukio haya , wadau mbalimbali wamekua wakijitokeza kusaidia kuondosha matatizo haya, nasi ni miongoni mwao tumeamua kujikita zaidi kielimu, tumeanza na mpango kazi wetu wa kutembelea madrasa mbalimbali visiwani Unguja kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na udhalilishaji kwa wanafunzi na walimu.

Jana tarehe 27 July 2019 tulifanikiwa kutoa elimu katika Al-madrasatul Muhaajirina iliyopo huko Mwera wilayani - Zanzibar.

Thursday, July 18, 2019

CHANGIA KUTENGENEZA AGHERA YAKO, WATOTO WAOZA MACHO NA USO


Assalam Alykum Warahmatullahi Wabarakatuh?

Hawa ni watoto kutoka kijiji cha Junguni, Wete Kisiwani Pemba nchni Tanzania (Zanzibar) ambao ni Husna na Riziki Hamadi , mmoja wa miaka 19 na mwengine miaka 6.

Siku chache zilozopita walipatwa na homa, badae wakaanza kuoza  macho kisha uso na mwili wote, wazazi wameshafuatilia matibabu katika hospitali tofauti lakini imeshindikana hasa kwakua hawana pesa za kujikimu katika matibatu.

Hali za familia ya watoto hawa kiuchumi ni mbaya sana, tunakuomba msaada wako kuchangia fedha kwa lengo la kuwapatia matibabu hata ikiwezekana nje ya nchi, tatizo kubwa ni hali mbaya kifedha na kama una uwezo wa kuwafanyia mpango matibabu wewe pia unakaribishwa.

Taasisi yako ya AZCA inabeba jukumu la kukuomba msaada kwa watoto hawa baadae kuwashuhulikia matibabu ili waendelee kuishi kwa Amani, kwani bado wanahitaji kusoma na kuishi vizuri, changia kwaajili ya ALLAH SUBHAANAHU WATAALA, SADAKA YAKO UTAIKUTA MBELE YA MUNGU.

Mawasiliano +255774181532 / +255774253759

Nambari ya kuchangia pesa (tigo pesa) +255672560173

Monday, July 8, 2019

MKUTANO WA KAMATI TENDAJI JULY 07,2019


Naibu Katibu mkuu wa All for Zanzibar Children Association - AZCA Salama Said Aboud akiwa makini kusikiliza kinacho changiwa na wanakamati tendaji wa jumuiya  katika kikao kilicho fanyika jana tarehe 07 july 2019 huko Vuga Mjini Zanzibar.

Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ikiwamo suala la kutafuta "jumuiya washirika" wenye malengo yanayofanana na taasisi ya AZCA.

Mwisho katika mkutano huo uliyowashirikisha wajumbe wa kamati tendaji hao , Naibu katibu Mkuu Salama Said aliwataka watendaji wote wa jumuiya

Saturday, July 6, 2019

Siku ya Mtoto wa Afrika

Juni 16 kila mwaka bara la Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tangu kuidhinishwa kwa siku hiyo na Umoja wa Afrika mwaka 1991. Umoja wa Afrika ulianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama sehemu ya kuwakumbuka na kutambua mchango wa watoto waliopoteza maisha katika mauaji yaliyotokea huko Soweto, Afrika ya Kusini wakati watoto walipoandamana kudai haki zao za msingi.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu huungana na jamii ya kiafrika kuadhimisha siku hiyo maalumu katika kutambua mchango wa watoto katika jamii, sambamba na kuamsha uelewa